Wasiwasi wachukua nafasi ya zawadi za Pasaka kwa famiia zinazo pitia wakati mgumu

The Foodbank popup store in Melbourne

The Foodbank popup store in Melbourne Source: AAP

Wakati wa Australia wengi wana jiandaa kwa likizo ndefu ya Pasaka, mashirika yamisaada ya chakula nayo yana jiandaa kwa muda wa shughuli nyingi zaidi ya mwaka.


Mkesha wa Ijumaa Kuu ya 2023 uliona idadi kubwa ya nyumba zinazo tegemea misaada ya mashirika kama Foodbank na Second Bite. Na idadi hizo zina onekana nikama zina ongezeka.

Unaweza samehewa kwa kufikiria kuwa krismasi ndio wakati wa mwaka wenye shughuli nyingi kwa mashirika yanayo toa msaada wa chakula.

Ila kwa mashirika mengi makubwa ya Australia, ni wakati unao karibia Pasaka, ambapo huduma nyingi ndogo za jumuia hufungwa kwa likizo ndefu na, kuna watu wachache wanao toa misaada ya bidhaa na hela taslim.

Na kwa ongezeko la bei ya chakula, mistari yakupokea chakula cha bure au cha punguzo ya bei ina endelea kuwa mirefu kote nchini, wakati familia moja kati ya tatu zawa Australia zina pata wakati mgumu kuweka chakula mezani.

Share