Taarifa ya Habari 23 Mei 2024

City - Swahili.jpg

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron yuko katika Kisiwa cha Pasifiki cha New Caledonia, kwa mazungumzo yenye lengo laku geuza ukurasa kwa ghasia mbaya iliyo chochewa na mageuzi ya uchaguzi unaopingwa. Watu sita wamefariki katika machafuko hayo na takriban watu 300 wamekamatwa.


Waandamanaji wanahofu mageuzi ya uchaguzi, ambayo yamepitishwa tayari na wabunge Ufaransa bara ambayo ni takriban kilomita 20,000 na kisiwa hicho, itapunguza nguvu ya kura yawatu wa asili wa Kanaks, ambao ni takriban asilimia 40 ya wakaaji wa kisiwa hicho chenye idadi ya watu 270,000.
Bw Macron amesema kipaumbele chake cha ziara yake nikusaidia kurejesha utulivu kisiwani humo, kisha kutafuta kiini cha machafuko hayo.

Maisha ya kituo cha nishati cha Australia kinacho tumia makaa ya mawe, yata ongezwa kwa angalau miaka mbili chini ya makubaliano ambayo yanaweza wagharimu walipa kodi wa New South Wales zaidi ya dola milioni 200 kila mwaka. Origin Energy imekuwa ikifanya mazungumzo na serikali ya New South Wales kuhusu, kuongeza muda wa matumizi ya kituo cha nishati cha Eraring baada ya tathmini kuonya ratiba yakustaafu ya Agosti 2025, inaweza sababisha uhaba wa umeme pamoja na ongezeko za bei. Wakati huo huo, Waziri wa nishati wa New South Wales Penny Sharpe amesema makubaliano hayo niya mpito na yanalenga kwa ajili yakutoa dhamana ya utaoji wakima cha chini cha umeme hadi tarehe mpya yakufungwa.

Data ya shughuli ya benki ya Commonwealth, imeonesha watu wenye umri katikati ya 20 nakuendelea wana endelea kuhisi uzito wa shinikizo ya gharama ya maisha. Data hiyo imefichua kuwa shinikizo ya kodi za juu pamoja na gharama zingine zinazo husiana, zime sababisha vijana wapunguze matumizi kwa asilimia saba katika mwaka hadi machi inapo rekebishwa kwa mfumuko wa bei. Takwimu hizo zina husiana na uchambuzi wa data ya shughuli ya benki ya commonwealth zilizo tambuliwa.

Rais wa Marekani Joe Biden alisema anapanga kufanya ziara rasmi barani Afrika mwezi Februari baada ya uchaguzi wa rais wa Marekani, tangazo ambalo linabashiri kuwa atamshinda Donald Trump. "Ninapanga kwenda mwezi Februari baada ya kuchaguliwa tena," Biden alisema alipokuwa akimsalimia Rais wa Kenya William Ruto alipowasili Ikulu katika siku ya kwanza kati ya mbili za mikutano na chakula cha jioni. Maafisa wakuu wa utawala walisema Biden na Ruto watajadili masuala mbalimbali kutoka biashara hadi msamaha wa madeni na njia ya kusonga mbele kwa ajili ya Haiti, Ukraine, Sudan na maeneo mengine. Biden, ambaye ni Mdemokrat, anawania muhula mwingine katika uchaguzi wa Novemba 5 dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Republican, Rais wa zamani Donald Trump.

Mamlaka ya Palestine ambayo kimataifa inatambuliwa kama mwakilishi rasimi wa watu wa Palestine imekaribisha hatua ya nchi za Ireland, Norway na Uhispania kutambua eneo hilo kama taifa, ikisema ni kitendo cha kihistoria. Kupitia taarifa yake kwenye mtandao wa X, katibu mkuu wa mamlaka hiyo Hussein al-Sheikh amesifia hatua hiyo ya , na .
Israel kwa upande wake imepinga vikali hatua hiyo, ikisema kuwa ni sawa na kitendo cha kigadi na kuunga mkono vitendo vya haswa baada ya kundi hilo kutekeleza shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel ambalo lilisababisha kuzuka kwa mapigano makubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye vita vya Gaza.

Katika mchezo wa  National Rugby League, mchezaji wa kimataifa wa New Zealand Isaiah Papali'i [[puppa-lee-ee]] ata ondoka katika timu ya Wests Tigers nakuhamia katika timu ya Penrith Panthers. Ametia saini mkataba wa miaka mitatu, na bingwa hao watetezi , kuanzia mwakani.

Share