Taarifa ya Habari 21 Mei 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Upinzani wa shirikisho umesema serikali haina "mpango wa kuaminika", kulinda mtandao wa umeme wa Australia kupitia kuhamia kwa nishati mbadala.


Ukosaji huo unajiri wakati opareta wa soko la nishati ya Australia AEMO, ametoa ripoti inayo onya kuwa mtandao wa umeme wa taifa uko katika hatari ya juu ya kukatika kwa umeme. Zaidi ya asilimia 60 ya vituo vya makaa ya mawe vya Australia, vinatarajiwa kufungwa kabla ya mwaka wa 2033. Ila ucheleweshwaji mkubwa wa miradi katika majimbo yanayo jumuisha Kusini Australia, Victoria na New South Wales, zina ongezeko ya hatari yakuaminika.

Viongozi wa majimbo tatu wame elezea nia zao zakuweka marufuku kwa matumizi ya mitandao yakijamii kwa watoto. Viongozi wa New South Wales, Victoria na Queensland wamekuja pamoja kuomba hatua zichukuliwe kuweka mahitaji ya chini ya umri kwa matumizi ya mitandao kama Facebook, X na Instagram. Hali hiyo imejiri wakati wa ongezeko la wasiwasi kutoka kwa wazazi kwa athari ya afya ya akili za watoto wao, kupitia maudhui ambayo hayaja chujwa yanayo furika katika majukwaa. Wakati huo huo kiongozi wa Kusini Australia Peter Malinauskas, ame dokeza kuwa jimbo lake lina nia yakuweka marufuku ya matumizi ya mitandao yakijamii kwa watoto wenye chini ya miaka 14.

Utafiti mpya umefichua kuwa wahamiaji na watoto wa wakimbizi wana uwezekano mkubwa zaidi wakuwa hatarini kupata matatizo ya maendeleo, kwa sababu ya upatikanaji mdogo wa elimu ya mapema ya utotoni. Utafiti huo uliofanya na chuo cha Kusini Australia kwa ushirikiano na Settlement Services International [[SSI]], ume onesha watoto kutoka asili mbalimbali, wana walikuwa na nusu ya uwezekano wakupokea miradi ya uingiliaji kati ya mapema kama, tiba yakuongea, tiba ya kazi au msaada wa ulemavu.
Watafiti wamesema kuwa udhaifu kwa maendeleo wanapo anza shule, unaweza sababisha mzunguko wakurudi nyuma nakuwa na madhara ya muda mrefu.

Mwendesha mashtaka mkuu kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Jumatatu amesema anataka kuomba hati ya kukamatwa kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa ulinzi Yoav Gallant, pamoja na kiongozi wa Hamas huko Gaza Yahya Sinwar kuhusiana na vita vya Israel na Hamas. Karim Khan amesema katika taarifa kwamba ofisi yake inaamini Netanyahu na Gallant “wana jukumu la uhalifu wa kivita dhidi ya ubinadamu, ikiwemo kuwatesa raia na njaa kama mbinu ya kivita na kuagiza kwa makusudi mashambulizi dhidi ya raia. Mbali na Sinwar, Khan alisema kamanda wa tawi la kijeshi la Hamas Mohammed Diab Ibrahim al-Masri na mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas Ismail Haniyeh pia wanahusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Khan amesema tuhuma dhidi ya maafisa wa Hamas ni pamoja na mauaji, kuwashikilia mateka kama uhalifu wa kivita, ubakaji na ukatili mwingine wa kingono, na mateso.

Viongozi wa dunia walokua wakihuddhuria mikutano mbali mbali wametoa heshima zao Jumatatu kwa kunyamaza kimya kwa dakika moja kumkumbuka rais wa Iran na washauri wake wa karibu waliofariki katika ajali ya helikopta siku ya Jumapili. Kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wajumbe walinyamaza kimya kabla ya kuanza kikao cha asubuhi kama ilivyotokea mjini Doha, Qatar kwenye mkutano wa Jopo na Usalama na kwenye makao makuu ya Idara ya Atomiki ya Umoja wa Mataifa mjini Vienna.

Mahakama ya juu ya Afrika Kusini imesema rais wa zamani Jacob Zuma anayekabiliwa na kashfa ya ufisadi hastahili kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa Mei 29. Zuma aliondoka madarakani mwaka 2018, akiandamwa na tuhuma za ufisadi, alifungwa jela kwa muda kwa kuidharau mahakama. Tangu wakati huo alianzisha chama cha kushindana na chama cha African National Congress cha mrithi wake Cyril Ramaphosa. Zuma na chama chake kipya, uMkhonto Wesizwe, tawi la zamani la kijeshi la ANC, walipinga uamuzi huo ambao sasa umeidhinishwa na mahakama ya katiba. Uamuzi wa Jumatatu unaweza kuwa na athari kubwa zenye misukusuko ya kisiasa.

Share