Taarifa ya Habari 24 Mei 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Ndege mbili za ziada zitatumika kutoka New Caledonia, serikali ya Australia ikiendeleza juhudi zakuwaleta nyumbani raia ambao wame kwama huko. Safari hizo za ndege ambazo zimefadhiliwa na serikali, zitaondoka kutoka eneo hilo la ufaransa katika Pasifiki leo Mei 24, baada ya zaidi ya wiki nzima ya migomo ambayo imesababisha vifo vya watu sita.


Chama cha Greens kime kosoa uamuzi wa serikali ya New South Wales kuunga mkono kifedha moja ya vituo vikubwa vya nishati ya makaa ya mawe vya Australia, kuhakikisha kina salia wazi kwa miaka mingine miwili. Serikali ya NSW itatumia takriban milioni $450 katika kituo cha umeme cha Eraring ambacho kiko Lake Macquarie ili kuhakikisha kiwango cha chini cha utoaji wa umeme kutoka kwa kituo hicho hadi mwisho wa 2027.
Vikundi vya mazingira vime kosoa matumizi ya hela za walipa kodi, kuimarisha nishati ya mafuta, ikisema ita zuia uingizwaji wa chini na sufuri.

Waziri wa afya wa Queensland Shannon Fentiman, me shtumiwa kwa kuchochea unyanyasaji wa mtandaoni baada yakuchangia video inayo dai upinzani ulimweleza "afunge miguu yake" bungeni. Msemaji wa afya katika upinzani Ros Bates amesema amepokea junge chafu pamoja na vitisho vya vurugu tangu, video hiyo iliposambaa katika mitandao ya kijamii. Video hiyo ilimwonesha Bi Fentiman akishambuliwa na upinzani kuhusu kufungwa kwa vyumba vya kuzaa vya kandani wakati wa maswali na majibu Jumatano.

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) itatoa uamuzi kesho juu ya hatua zaidi za kisheria za kuzuia mauaji ya halaiki ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kwa kujibu ombi la Afrika Kusini. Mahakama hiyo ya ICJ, imesema leo kwamba uamuzi huo utatangazwa wakati wa kikao cha umma kwenye kasri ya Amani mjini The Hague nchini Uholanzi hapo kesho mchana. Jaji msimamizi wa mahakama ya ICJ Nawaf Salam atasoma uamuzi huo.
Uamuzi huo unahusu ombi la Afrika Kusini la Mei 10 mwaka huu kuhusu matumizi ya Mkataba wa Kuzuia na Adhabu ya Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza pamoja na ombi la dharura la Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) kujiondoa kwenye mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza. Ingawa maamuzi ya mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa yanafunga kisheria, mahakama hiyo haina njia ya kulazimisha kutekelezwa kwake. Hata hivyo, inaweza kutoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukuwa hatua.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, juma hili ameendelea kusisitiza kuwa nchi yake ni salama kwa wahamiaji wanaotarajiwa kupelekwa nchini humo kutokea Uingereza, Kagame akiwanyooshea kidole wanaokosoa mpango wa mataifa hayo mawili. Haya yanajiri wakati huu tayari baadhi ya raia wameanza kupelekwa nchini humo, baada ya bunge kupitisha sheria iliyokuwa na utata kuhusu uhamiaji na waomba hifadhi. Kauli yake anaitoa wakati huu watetezi wa masuala ya haki za binadamu, wakifungua kesi mpya kutaka mpango huo kusimamishwa.

Rais William Ruto wa Kenya amesema kuwa ni muhimu kufanya mfumo fedha wa kimataifa uwe mwepesi zaidi ili kuzisaidia nchi kupambana na majanga, na karibisha uungaji mkono wa Marekani wa kufanya mageuzi kama hayo. Akizungumza Alhamisi wakati wa kuanza mkutano wa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Marekani Joe Biden, Ruto amesema hivi karibuni aliitisha mkutano wa kilele kwa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Benki ya Dunia kuzungumzia suala la madeni ya mataifa mengi yenye kipato cha chini. Amesema lengo lilikuwa kutafuta njia za kufanya taasisi za fedha kuwa “nyeti, haraka na kuweza kujibu matatizo yanayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa, mfumko wa bei na viwangi vya riba.”

Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya Kimataifa ya kuzuia Fistula hali ambayo wanawake wanashindwa kuzuia haja, baada ya kujifungua na kusababisha harufu mbaya, nchini Sudan Kusini, wanawake zaidi ya Elfu Sita wanasumbuliwa na tatizo hilo kila mwaka, kwa mujibu wa Wizara ya afya. Mara nyingi kinachotokea ni kwamba wanawake walio vijijini huzuiwa na wakunga wa kienyeji kwenda hospitalini kwa sababu wanaamini kuwa ni sharti wanawake wajawazito wajifungulie nyumbani kwa njia ya kawaida na hawapaswi kufanyiwa upasuaji katika vituo vya afya, hii imesababisha wengi kuathiriwa baada ya kuamua kujifungua wakiwa nyumbani.

Share