Wanafunzi walengwa kuwa wasafirishaji wa pesa na wanakabiliwa na madhara makubwa

money_aap.jpg

Get the SBS Audio app

Other ways to listen

Kuna onyo mpya kuhusu matangazo yakufanyia kazi nyumbani, ambayo yanaonekana kuvutia sana au yanayo ahidi maokoto makubwa kwa uwekezaji.


Matangazo mengi yanajaribu kuajiri ‘wasafirishaji wa hela’. Jeshi la Polisi la shirikisho na taasisi zaki fedha, zimesema makundi mengi yawahalifu yanawalenga wanafunzi wawe wasafirishaji wa hela.

Wakati uhalifu wamtandaoni unaweza kuwa na umbo mbali mbali, moja ya wasiwasi kubwa si tu kwa wa Australia ila, pia uko kwa wanafunzi ambao ni wageni nchini.

Baadhi ya benki hivi karibuni ziliwasilisha mifumo mipya yaku tambua akaunti za benki zawasafirishaji wa hela, katika kile wanacho ita tatizo linalo endelea kukuwa kote nchini Australia.


Share