Umuhimu wa kuelewa tofauti zakitamaduni miogoni mwa wa Australia wa kwanza

Portrait of three generation Aboriginal family

Portrait of three generation Aboriginal family Credit: JohnnyGreig/Getty Images

Kuelewa utofauti ndani ya jumuiya yawa Australia wa Kwanza ni muhimu unapo jihusisha nawa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait pamoja nakujenga mahusiano yenye maana.


Key Points
  • The Indigenous peoples of Australia are not one homogenous group.
  • There are around 500 Nations, each with different cultures, languages, ways of life and kinship structures.
  • Understanding this diversity is crucial to building meaningful relationships with the Indigenous peoples.
Utajiri wa utofauti uliomo ndani ya watu wa asili wa Australia ni kitu chakuvutia sana, kitu kinacho pinga dhana potofu kuwa wa Aboriginal wote na wanavisiwa wa Torres Strait ni watu wa kundi moja.

Watu wa asili huwakilisha tamaduni, lugha, aina ya maisha na mifumo ya ukoo.

Moja ya njia bora yaku kumbatia utofauti huu nikutazama , kama anavyo elezea Aunty Munya Andrews, yeye ni kiongozi kutoka nchi ya Bardi ambayo iko katika kanda ya Kimberley Magharibi Australia.

“Tunawakaribisha watu waitazame kwa sababu kuna takriban mataifa 500 kwenye ramani hiyo. Kila taifa ina lugha yake au inachangia lugha na taifa lingine.”
_Carla-and-Aunty-Munya.jpg
Carla Rogers (left) and Aunty Munya Andrews (right), Evolve Communities Credit: Evolve Communities
Kuna zaidi ya lugha 250 zawatu wa asili, zinazo jumuisha lahaja 800, tamaduni zao, hali ya maisha na miundo ya jamaa inatofautiana katika mataifa yote, hata sanaa zao pia ameongezea Aunty Munya.

“Naweza jua kwa kuangalia tu sanaa yaki Aboriginal, najua haswa inatoka wapi nchini Australia. Ni maalum hivyo. Watu wengi hu husisha michoro ya nukta na tamaduni yawa Aboriginal ila, hilo ni taifa moja tu.

“Unapo watazama watu wa Bardi, watu wangu, sisi ni watu wa maji ya chamvu, sanaa yetu ni sawia na ile yawana visiwa wengine kote duniani,ni michoro yakijiometria inayo onesha mawimbi nasi michoro ya nukta kabisa,” alisema.

Aunty Munya, ni mwandishi, mwanasheria na mkurugenzi mwenza wa shirika la Evolve Communities, amesema watu wanastahili elewa kuwa ‘watu wa asili wote hawako sawa inapokuja kwa kushughulika na watu wa asili.

Ni hatua muhimu kwa kuonesha heshima kwa mila na tamaduni ya jamii, kukuruhusu kujenga mahusiano mengi yenye maana.

Carla Rogers ni mshiriki wa waastralia wa kwanza na yeye hufanya kazi pamoja na Aunty Munya. Ameongezea kuwa ujuzi kama huo ni muhimu kuelea historia ya Australia inayo changiwa na kwanini mapengo yako kati ya watu wa asili na wasio wa asili hadi leo.

“Australia ilipokuwa chini ya ukoloni kwa mara ya kwanza na kuendelea, ni uhaba wa uelewa wa utofauti huu ambao ulikuwa kitovu cya tatizo letu. Matatizo yetu mengi yaliyopo kwa sasa, ni kwa sababu yakuona wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait kama kundi moja na kuto kiri utofauti huo tajiri,” amesema.
Multigenerational Aboriginal Family spends time together in the family home
The Indigenous peoples of Australia are not one homogenous group. - Belinda Howell/Getty Source: Moment RF / Belinda Howell/Getty Images

Australia daima imekuwa na tamaduni nyingi

Watu wa asili ni "wataalam" katika utamaduni mwingi, Aunty Munya amesema.

“Watu wangu wame kuwa waki shughulika na tamaduni nyingi kwa maelfu ya miaka. Tumejifunza kushirikiana na makundi mengine yawa Aboriginal, kujifunza kuzungumza na katika nchi zingine,” ame elezea.

Ni muhimu kuwatambua watu kama Dr Mariko Smith, ambao wana asili yawatu wa asili na tamaduni, kwa hiyo kuboresha utofauti wa waAustralia wa kwanza.

Babake anatoka katika Taifa la Yuin, katika pwani ya kusini ya New South Wales, wakati mamake anatoka Kokura ambayo iko Kyushu, Japan.

“Baadhi ya watu hufikiri kwa sababu ya asili yangu ya Japan nau Aboriginal kuwa, natoka kaskazini na kaskazini magharibi Australia, ambako kulikuwa wajapani katika sekta ya madini ya pearl.

“Ila wazazi wangu walikutana ndani ya duka la kahawa mjini Kyushu babangu alipokuwa akisafiri nchini Japan. Wali fanyia harusi Japan kisha alimleta Australia.”

Dr Smith alipitia uzeofu wa “matusi ya ubaguzi wa rangi” alipokuwa aki kuwa, kwa kufanana na watu kutoka Asia, ila amesema matusi hayo yali “enda katika kiwango kingine” wakati watu walipata kuwa yeye nimu Aboriginal.
Unsettled_Weekend
Dr Mariko Smith Credit: Anna Kucera Credit: Anna Kucera/Anna Kucera
Ni kwa sababu ya mitazamo na mitazamo finyu ambayo watu wanayo kuhusu wa Aboriginal, kama rangi ya ngozi au kiwango cha ustaarabu wanayo jifunza kutoka historia iliyo andikwa, Dr Smith ame elezea.

“Watu wanaweza dhani kuwa hawaja kutana na mtu waki Aboriginal kabla katika maisha yao ila, kuna uwezekano wame kutana naye tayari, pengine wahawaja thibitisha kwa mitazamo ya dhana za watu.”

Dr Smith amesema kuwa Australia ya kisasa, yenye tamaduni nyingi lazima itambue na ikumbatie utofauti uliopo ndani ya umma yawa Australia wa kwanza ili iwe jumuishi kwa kweli.

“Kama unafikiria kuhusu watu waki Aboriginal, katika njia rahisi sana, basi kutakuwa suluhu rahisi tu. Ni dhana tata, tofauti inayo hitaji suluhu tofauti naza kina na, zinazo fikiriwa vizuri pia.”

Carla Rogers ame elezea kuwa watu wanaweza fanya makosa wakati watu ambao si wa asili hawa elewi utofauti huu.

“Tunaweza sema kitu ambacho kinaweza umiza sana, kitu ambacho kina uwezekano wakuwa ubaguzi wa rangi. Ni kizuizi kuelewa.”
Thirteen Aboriginal and Torres Strait Islander people from across Australia taking part in the inaugural Mob in Fashion initiative.
Thirteen Aboriginal and Torres Strait Islander people from across Australia are taking part in the inaugural Mob in Fashion initiative. Credit: Thirteen Aboriginal and Torres Strait Islander people from across Australia are taking part in the inaugural Mob in Fashion initiative.

Tunaweza jifunzia mengi zaidi wapi kuhusu utofauti wa waAustralia wa kwanza?

Kama unavyo weza fanya unapo safiri Uingereza, anza kwa ramani, tambua nchi ambako uko na jifunze kuhusu tamaduni na lugha.

“Kama unasafiri zaidi ya masaa mawili, tuseme kutoka Sydney, kisha unapitia katika nchi tofauti,” Rogers amesema.

Kupata uelewa wa kina kwa nchi, kujumuisha wamiliki wayo wa jadi na historia, Land Council ni sehemu nzuri zakuanzia.

Aunty Munya amesema inahusu “kuji elimisha”.

“Jifunze uwezavyo, jumuika, haswa nawa Australia wa kwanza. Hakuna haja yakuogopa, jiwasilishe, nenda katika matukio ya jamii.”

Ina husu kuwa mjasiri yakutosha, kuchukua hatua hiyo kuwajua wa Australia wa Kwanza.

Share