Taarifa ya Habari 4 Machi 2024

City - Swahili.jpg

Waziri mkuu Anthony Albanese amesema uchaguzi mdogo wa Dunkley umethibitisha kuwa wa Australia hawa vutiwi na kampeni hasi.


Mbunge wa chama cha Liberal Sussan Ley amekosolewa kwa ujumbe alio andika katika mtandao wa X kabla ya kura kupigwa, ulio sema "kama hautaki wanawake wa Australia wanyanyaswe na wahalifu wakigeni, piga kura dhidi ya Labor".** Bw Albanese ame eleza shirika la habari la radio 5-A-A kuwa, jumuiya haipendi aina hiyo ya maneno.

Adui mkubwa wa jeshi la ulinzi la Australia yuko ndani yake, amesema mwenye kiti wa tume yakifalme iliyo pata kuwa jeshi la taifa lina kabiliana na maswala ya kina yakitamaduni. Alipo fungua vikao vya mwisho vya umma vya tume yakifalme katika visa vya kujiuwa vya wanajeshi wastaafu, Mwenyekiti Nick Kaldas aliomba ushirikiano na uwajibikiaji kushughulikia changamoto zakimfumo. Bw Kaldas amesema uchunguzi huo haujakuwa ukitaka kudhoofisha uwezo au kukosea heshima historia yakifahari ya jeshi la Australia.

Kuimarisha mahusiano yaki uchumi, usalama wakikanda, mabadiliko ya mazingira na nishati safi, viko juu ya ajenda ya viongozi wanao jumuika kwa kongamano maalum la ASEAN-Australia mjini Melbourne. Viongozi wanao hudhuria mkutano wa chama cha mataifa ya Kusini mashariki ya Asia, watafanya mkutano baina ya nchi hizo juu ya ratiba iliyo jaa pamoja na kufanya majadiliano katika muda wa siku tatu kuanzia leo 4 Machi.

Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris Jumapili alitoa wito wa sitisho la mara moja la mapigano katika ukanda wa Gaza na kuishinikiza kwa dhati Israel kuongeza usambazaji wa misaada ili kupunguza kile alichokiita “hali isiyo ya kibinadamu” na “janga la kibinadamu” miongoni mwa Wapalestina. Harris, ambaye alikuwa akizungumza kwenye hafla huko Selma jimbo la Alabama, kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji mabaya au “Bloody Sunday”, ambapo wanajeshi wa jimbo hilo waliwapiga watu waliokuwa wakiandamana kwa amani, aliihimiza Hamas kukubali makubaliano ya kuwaachia huru mateka ambayo yatakuwa mwanzo wa sitisho la mapigano kwa kipindi cha wiki sita na kuruhusu usambazaji wa misaada kwa wingi. “Watu wa Gaza wanakabiliwa na njaa. Hali ni ya kinyama na ubinadamu wetu wa pamoja unatulazimisha kuchukua hatua,” Harris alisema. “Serikali ya Israel lazima ifanye juhudi zaidi kwa kuongeza vya kutosha usambazaji wa misaada kwa wingi. Hakuna visingizio hapa.”

Familia ya mbunge Cherubin Okende aliyeuwawa nchini Kongo miezi saba iliopita imepinga ripoti ya uchunguzi wa mwendesha mashtaka iliyohitimisha kwamba mwanasiasa huyo w aupinzani alikufa kwa kujitoa muhanga. Akizungumza na waandishi habari mjini Kinshasa, mwendesha Mashtaka Mkuu, Firmin Mvonde, alitangaza kwamba Chérubin Okende alijiua kwa kujipiga risasi. ''Uchunguzi ulihusu matumizi ya risasi, mawasiliano, mwili wa marehemu na madakatari wa upasuaji wa maiti. Na uchunguzi wa maiti unaonyesha Okende alikufa kufuatia na kuvuja damu kutokana na kidonda kilichosababishwa na silaha aliyotumia mwenyewe." Kauli hii inakuja ikiwa ni sehemu ya kesi inayohusu kifo cha aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, aliyepatikana amefariki kwenye gari lake Julai 13, 2023 huko Kinshasa. Kulingana na hitimisho la uchunguzi, alijiua mwenyewe, kwa kujipiga risasi kwenye kichwa chake. Ripoti hiyo ya uchunguzi imefuta nadharia kadhaa juu ya tukio hili. Kwanza ripoti ya uchunguzi inaeleza kuwa Okende hakuwepo siku moja kabla ya kifo chake saa kumi alasiri katika Mahakama ya Katiba. Simu yake wakati huo ilionekana katika mtaa mwengine mbali na mahakama ya katiba.

Mchekeshaji maarufu wa Nigeria, John Okafor almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia siku ya Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mrefu. Bw. Ibu alifariki akiwa katika hospitali moja mjini Lagos alipokuwa akipatiwa matibabu. Rais wa Chama cha Waigizaji wa Filamu wa Nigeria, Emeka Rollas alithibitisha taarifa za kifo cha Bw. Ibu siku ya Jumamosi.

Katika michezo,
Ligi kuu ya NRL ime anzia mjini Las Vegas, Marekani ambako Manly Sea Eagles ime anza kwa kuishinda Souths Sydney Rabbitohs 36-24. Katika mechi nyingine Sydney Roosters ime icharaza Brisbane Broncos 20-10

Nyota wa soka ya ligi kuu ya Uingereza, ame isaidia timu yake kupata ushindi wa magoli matatu kwa moja katika debi ya Manchester usiku waku amkia leo. Phil Foden mwenye miaka 23, aliongoza timu yake katika mechi ya kusisimua, kwa kufunga magoli mawili katika mechi hiyo ya ligi kuu dhidi ya watani wao wajadi. Punde baada ya mechi hiyo, mwalimu wa Manchester City Pep Guardiola, amesema Foden ameonesha kiwango chakuwa gwiji wa mchezo huo.

Na katika taarifa za utabiri wa hali ya hewa:

Adelaide nyuzi joto 29
Brisbane nyuzi joto 30
Canberra nyuzi joto 23

Hobart nyuzi joto 20
Melbourne nyuzi joto 22
Sydney nyuzi joto 24
Perth nyuzi joto 27

Share