Taarifa ya Habari 27 Februari 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Asilimia 90 au zaidi ya waajiri katika sekta za madini, umeme, maji, huduma za taka, fedha na bima, wana pengo la malipo linalo wapendelea wanaume.


Shirika linalo shughulikia maswala ya usawa wa jinsia kazini, lime chapisha mapengo wastan ya malipo ya jinsia kwa takriban waajiri elfu 5 wa sekta binafsi ya Australia yenye wafanyakazi 100 au zaidi.

Baadhi ya wanachama wa Jumuiya ya Wanyarwanda wanao ishi Australia, wame eleza shirika la habari la SBS kuwa wana hofia maisha yao kwa sababu wana amini wana lengwa na mtandao wa wajasusi walio sajiliwa na serikali ya Rwanda. Huu ni mwaka wa 30 wa mauaji ya kimbari ya Rwanda na, uchaguzi mkuu utakuwa nchini Rwanda Julai, baadhi ya wanachama wa jumuiya hiyo wamesema matukio hayo yamesababisha ongezeko la vitisho na ukandamizaji wa ukosoaji wa serikali ya Rwanda.

Wazima moto jimboni Victoria wala lenga kuzuia vifo wakati jimbo hilo lina jianadaa kukabiliana na hali mbaya ya mazingira ya hewa. Viwango vya hatari ya moto katika kanda ya Wimmera kwa kesho ((Februar i28)) vimeongezwa kutoka hali iliyo kithiri hadi janga, hatari ya moto imetabiriwa kwa wilaya tisa za Victoria kufikia katikati ya wiki hii. Upepo wenye kasi ya 45km kwa saa unatarajiwa, na sehemu nyingi za jimbo hilo zinatarajia kufikia nyuzi joto 40.

Msemaji wa serikali ya Burundi amesema Jumatatu kwamba watu wenye silaha kutoka kundi la waasi la Red Tabara wameua watu 9 na kujeruhi wengine kwenye mashambulizi ya usiku kucha magharibi mwa mwa nchi karibu na mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Red Tabara limekuwa likipigana na serikali ya Burundi kutoka kwenye vituo vyake ndani ya Congo tangu 2015. Kupitia ujumbe wa X iliojulikana kama Twitter, Red Tabara limesema kwamba limeshambulia vituo viwili vya kijeshi vya Burundi Jumapili usiku, wakati likiteka silaha pamoja na risasi, na kwamba wanajeshi 6 waliuwawa.

Serikali inayoongozwa na jeshi nchini Sudan imezuia misaada inayopelekwa katika la eneo la Darfur Magharibi, hatua iliyozusha shutuma kali kutoka kwa wafanyakazi wa misaada na Marekani. Umoja wa Mataifa umelazimika kupunguza shughuli zake za kuvuusha msaada huo kutoka Chad kuelekea Darfur.
Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Eddie Rowe, aliwaambia waandishi habari kwamba mamlaka nchini Chad imezuia operesheni hiyo ya kuvuusha misaada.

Mazoezi ya kijeshi yanayoongozwa na Marekani kwa jina "Justified Accord" yanaanza nchini Kenya Jumatatu, huku zaidi ya mataifa 20 yakishiriki katika tukio ambalo limetajwa kuwa kubwa zaidi la aina yake katika Afrika Mashariki. Zoezi hilo la siku 11, ambalo litakamilika Alhamisi ijayo, linalenga kuongeza utayari wa nchi shiriki kwa misheni za kulinda amani, kukabiliana na janga na usaidizi wa kibinadamu, kulingana na shirika la utangazaji la serikali la SNTV na vyombo vya habari vya Kenya.


Share