Taarifa ya Habari 26 Februari 2024

City - Swahili.jpg

Vikwazo vyakifedha vya mtindo wa Magnitsky pamoja na marufuku yakusafiri, yametolewa dhidi ya maafisa saba wa gereza ambao serikali ya Australia ina amini, walishiriki katika unyanyasaji wa


Alexei Navalny ndani ya gereza moja nchini Urusi. Naibu waziri Mkuu Richard Marles na naibu waziri wa maswala yakigeni Tim Watts, wame toa taarifa yapamoja inayo thibitisha vikwazo hivyo. Wamesema vikwazo hivyo ni hatua inayo fuata katika juhudi za Australia kuwajibisha walio husika katika kile inacho ita "ukiukwaji mubaya wa haki za binadam za Bw Navalny".

Wajenzi wanao fanya kazi ndani ya bunge la taifa, wame zindua mgomo wa masaa 24, kwa sababu ya malipo yao. Chama kinacho wakilisha wafanyakazi wa umeme kimejiunga na chama cha wafanyakazi wa uzalishaji na CFMEU, nje ya bunge la taifa kwa maandamano yakuanza mgomo huo, wakati wanasiasa walikuwa wakijumuika katika mji mkuu wa taifa. Chama cha ETU kimesema baadhi ya wafanyakazi katika bunge la taifa hulipwa takriban $30,000 chini ya kigezo cha sekta hiyo kwa kazi wanayo fanya katika idara ya huduma za kwanza. Brad Pidgeon ni kaimu katibu wa tawi, amesema mazungumzo yaku suluhisha mzozo huo, hayaja zaa matunda kufikia sasa.

Wataalam wanatabiri kutakuwa kura dhidi ya chama cha Labor katika uchaguzi mdogo ujao wa Victoria. Kura mbili za maoni za magazeti ya Nine Resolve Political Monitor, na Newspoll ya The Australian, zime dokeza kuwa chama cha Labor kime poteza uvutio wayo kwa kura ya kwanza katika eneo bunge la Dunkley, ambalo liko Victoria. Eneo bunge hilo lili simamiwa na mbunge wa chama cha Labor Peta Murphy hadi alipo fariki baada yaku kabiliana na saratani ya matiti mwaka jana. Kura ya maoni ya Resolve imeonesha kuwa chama cha mseto kina asilimia 37 ya wapiga kura dhidi ya asilimia 34 ya chama cha Labor, wakati huo huo matokeo ya kura ya maoni ya Newspoll yana onesha kuwa chama cha Mseto kina ongoza kwa asilimia 36 ya kura dhidi ya Labor ambayo ina asilimia 33.

Raia 15 waliuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi kwenye kanisa katoliki wakati wa ibada ya Jumapili kaskazini mwa Burkina Faso, afisa kwenye kanisa hilo alisema. “Tunataka kuwafahamisha kuhusu shambulio la kigaidi ambalo lililenga jamii yetu ya kikatoliki katika kijiji cha Essakane Februari 25, wakati waumini walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya ibada ya Jumapili,” kasisi wa dayosisi ya Dori, Jean Pierre Sawadogo alisema katika taarifa iliyowasilishwa kwa shirika la habari la AFP. .Idadi ya awali ni ya watu 15 waliouawa na wawili waliojeruhiwa, aliongeza.

Aliyekuwa rais wa Namibia Hage Geingob ambaye alifariki akiwa hospitalini  Februari 4, wiki kadhaa baada ya kupatikana na saratani, amezikwa kwenye bustani ya mashujaa ya Heroes Acre, Jumapili, huku maelfu ya watu wakihudhuria wakiwemo viongozi 25 wa mataifa, pamoja na marais wa zamani. Mazishi hayo yamefanyika viungani mwa mji mkuu wa Windhoek, baada ya siku 20 za maombolezo, huku wanajeshi wakifyatua mizinga 21 kwa heshima yake, wakati ndege za kivita za kijeshi zikipaa angani kwenye eneo hilo. Geingop aliyekuwa na umri wa miaka 82 aliwahi kuwa waziri mkuu wa taifa hilo mara mbili, na baadaye kuwa rais wa 3 wa taifa hilo tangu kujipatia uhuru wake kutoka Afrika Kusini 1990. Utawala wake wa taifa hilo lenye watu wachache na ambalo sehemu kubwa ni jangwa, ulianza 2015.

Katika michezo,
Mwendesha baiskeli wa Australia, Ben O'Connor amepoteza ushindi katika mashindano ya UAE, alipoteza uongozi wa mashindano hayo kwa sekunde mbili dhidi ya Lennert van Eetvelt. Van Eetvelt mwenye miaka 22, aliongeza juhudi katika dakika ya mwisho mashindano hayo kumpiku O’Connor aliye maliza katika nafasi ya pili kwa ujumla. Mu Australia huyo ali elezea masikitiko yake kwa matokeo hayo ila, amesema mshindani mwenye nguvu zaidi alishinda na nafasi ya pili bado ni mafanikio.

Liverpool FC ime nyanyua kombe la Carabao katika dimba la Wembley dhidi ya wapinzani wao Chelsea FC, vijana wa Anfield wali pata ushindi wa goli moja kwa sufuri kupiptia nahodha wao van Dijk katika dakika 30 za nyongeza.

Share