Taarifa ya Habari 23 Februari 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Get the SBS Audio app

Other ways to listen

Muda wastan unao hitajika kuokoa asilimia 20 ya hela zaku nunua nyumba ume pungua.


Kwa wana ndoa wanataka nunua nyumba yao ya kwanza, kampuni ya Domain real estate, imesema watu wata okoa miaka minne na miezi tisa kwa wastan kote nchini. Hiyo ni miezi mbili michache kuliko ilivyo kuwa na inajiri licha ya bei za juu za nyumba. Muda waku weka hela zaku nunua nyumba ndani ya gorofa ume pungua pia.

Serikali ya shirikisho imetangaza kuwa ita toa uwekezaji wa $3 milioni kwa mradi unao lenga kuongeza uelewa wa ishara za vurugu na jinsi yakukabiliana na ufichuzi wa unyanyasaji. Ina lenga haswa viongozi wakidini na jumuiya zenye tamaduni na lugha mbali mbali katika juhudi yakumaliza uhalifu dhidi ya wanawake na watoto. Kwa wastan nchini Australia mwanamke mmoja kila wiki hu uawa na mpezi wake wa sasa au wa zamani, wakati wanawake wawili kati ya watano wamepitia uzoefu wa vurugu tangu umri wa miaka 15.

Shirika la New South Wales Health lime toa onyo kwa watu wawe waangalifu kwa dalili za ugonjwa wa Legionnaires'. Onyo hilo linatumika kwa mtu yeyote aliyekuwa katika maeneo ya karibu ya Victoria Park katika eneo la Camperdown katika siku 10 zilizo pita.
Ugonjwa wa Legionnaires' ni aina ya nimonia inayo sababishwa na bakteria ya legionella, ambayo ni tisho kwa maisha ila si kawaida.

Brazil imesema kuwa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G20 wanaunga mkono suluhisho la mataifa mawili kwa mzozo kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas katika ukanda wa Gaza. Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alikuwa amemtaka Vieira kutumia hotuba yake ya mwisho kwenye mkutano huo kuuelezea ulimwengu kwamba katika mkutano huo wa G20, kila mtu alikuwa anaunga mkono suluhisho hilo la mataifa mawili kwa kuweko kwa taifa huru la Palestina pamoja na lile la Israel.

Maelfu ya raia waishio kwenye mji wa GOMA mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya kongo, wanahangaika hivi sasa kutokana na upungufu mkubwa wa chakula ndani ya maduka na masoko ya eneo hilo. Hali hiyo inashuhudiwa baada ya waasi wa M23 kuzifungwa barabara muhimu zinazo sambaza bidhaa katika mji huo.

Lugha ya Mama au lugha ya asili ni msingi imara wa kujifunza lugha nyingine. Kwasababu ni lugha ya kwanza ambayo mototo anajifunza nyumbani kabla ya kuanza masomo. Wataalamu na wadau wa lugha ya Kiswahili nchini Tanzani na Kenya wamesema lugha za asili ni muhimu kwa watoto wafundishwe kabla ya kuanza masomo ili kuikuza lugha ya Kiswahili yenye maingiliano na lugha hizo za asili za Kiafrika.

Mamia ya waombolezaji nchini Kenya, Alhamisi wamesindikiza jeneza la mwanariadha bingwa wa dunia wa mbio ndefu Kelvin Kitum, wakati lilipokuwa likipekekwa kwenye kijiji chake ambako atazikwa.



Share