Taarifa ya Habari 22 Februari 2024

City - Swahili.jpg

Get the SBS Audio app

Other ways to listen

Uhaba wa ushindani sokoni waifanya serikali ya shirikisho izindue uchunguzi wa swala hilo.


Serikali ya shirikisho ina wasiwasi kuhusu uhaba wa ushindani katika uchumi wa Australia. Afueni ya gharama ya maisha imekuwa kipaumbele cha ajenda yaki siasa mwaka huu, ripoti mpya iliyo agizwa na Baraza la vyama vya biashara ya Australia, ilipata kuwa uhaba wa ushindani ulikuwa una ongeza mfumuko wa bei. Serikali ime agiza tathmini kwa kanuni ya chakula na mboga na, ime agiza pia kampuni inayo shughulikia maswala ya watumiaji Choice, itoe ripoti za kulinganisha bei za vyakula za biashara mbali mbali kila robo.

Kukabiliana na ongezeko la wasiwasi miongoni mwa jumuiya zenye lugha na tamaduni tofauti kuhusu jinsi wanaweza linda taarifa zao, ID Support New South Wales ina zindua mafunzo katika lugha ya mama kwa watu wanao zungumza Kiarabu na Kivietnam. Lengo la mafunzo hayo niku elimisha watakao hudhuria kuhusu jinsi yakutambua walaghai, kadi za mikopo pamoja na usalama wa neno zao za siri na wataalam wata kuwa hapo kujibu maswali yao. Shirika la ID Support NSW limesema watu ambao hawazungumzi kiingereza nyumbani, wako hatarini zaidi kwa mashambulizi ya programu hasidi za kompyuta, wizi wa utambulisho na ulaghai.

Mafunzo hayo yatafanywa katika maktaba ya Fairfield 22 Februari katika Kiarabu na ndani ya Maktaba ya Cabramatta 29 Februari katika lugha yaki Vietnam. Mnamo 2022, jumuiya zenye lugha na tamaduni mbali mbali, zilijumuisha karibu 5% ya ripoti kwa shirika la Scamwatch ambalo huchunguza maswala ya ulaghai, zikiwa zimepoteza takriban $56.6 million.

Maeneo saba ya ziada jimboni NSW yame tambuliwa kuwa yana asbestos, hospitali ya watoto pamoja na kituo cha wazima moto ni miongoni mwa sehemu hizo. Wakati sampuli moja ilipatwa kuwa na uwezekano wa asbestos inayo weza kauka, aina ya asbestos ambayo haina madhara makubwa ili gunduliwa pia ndani ya mbolea katika vitongoji kadhaa vya magharibi ya mji wa Sydney na kusini magharibi. Hali hiyo inafikisha idadi ya maeneo yaliyo athiriwa kuwa 54, wakati maeneo mengine 801 yame rejesha vipimo hasi tangu asbestos ilipo patikana ndani ya mbolea iliyo chakatwa katika eneo la Rozelle Parklands mwezi wa Januari.

Huduma za dharura za Victoria zina jiandaa kukabiliana na hali mbaya zaidi ya mazingira, wiki moja baada ya moto wa vichaka na dhoruba kuharibu mali nakuacha nyumba nusu milioni pamoja na biashara bila umeme. Nyuzi joto zina tarajiwa kupita 40 katika sehemu za jimbo hilo, na dhoruba zinatarajiwa baadae leo Alhamisi, zikiwa na upepo wa kasi ya 80km kwa saa pamoja na radi kavu. Marufuku kamili ya moto imetangzwa kwa kanda sita za Victoria, maeneo kama Mallee, Wimmera, Northern Country, North Central, South West na Wilaya ya kati ziki kabiliwa kwa viwango hatari vya moto. Onyo kali za moto zime tolewa pia kwa majimbo ya Kusini Australia, Tasmania na Magharibi Australia, ambako huduma za dharura zime kuwa ziki kabiliana na mioto tangu mwanzo wa msimu wa majira ya joto.

Spika wa bunge la Cuba Esteban Lazo anatembelea Nairobi kwa lengo la kupata maelezo bayanajuu ya hatma ya madaktari wawili wa Cuba waliotekwa nyara nchini Kenya na wanamgambo wa Somalia takriban miaka mitano iliyopita. Katika taarifa wizara ya mambo ya nchi za nje mjini Havana, inaeleza kwamba ziara ya mjumbe maalum Lazo unafanyika baada ya Al-Shabab kutoa taarifa ya Al- Shabaab kwamba madaktari hao wawili wameuawa kutokana na shambulio la anga la Marekani wiki iliyopita. Lazo “amekwenda Kenya kwa lengo la kushiriki katika utaratibu wa dharura na maafisa waandamizi wa nchi hiyo,“ imeleza taarifa ya wizara iliyochapishwa Junanne.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limetangaza vikwazo dhidi ya viongozi sita wa makundi ya waasi wanaopigana mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Kati yao ni msemaji wa kundi la M23 Meja Willy Ngoma.
Wengine ni viongozi wa kundi la Allied democratic forces na FDLR wakiwiemo Apollinaire Hakizimana, Ahmad Mamood, Mikel Rukunda, Mohamed Ali Nkalubo, na William Amuri. Vikwazo vinawazuia kupata silha, mafunzo, msaada wa kifedha na kusafiri. Taarifa ya baraza la usalama la umoja wa mataifa inasema kwamba Ngoma amelengwa kwa kuwa mmoja wa viongozi wa kisiasa na kijeshi wa kundi la waasi la M23 linaloshutumiwa kwa vita, mauaji na mateso ya raia mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Waasi wa M23 wanaoripotiwa kuungwa mkono na Rwanda wamekuwa wakipigana na wanajeshi wa DRC wakitaka kudhibithi mji wa Sake karibu na Goma.

Share