Taarifa ya Habari 20 Mei 2024

City - Swahili.jpg

Serikali ya Albanese imetetea hatua zakutoa afueni kwa gharama ya maisha, licha ya bajeti ya shirikisho kuipa serikali jeki ndogo katika kura za maoni.


Kura ya maoni kutoka kampuni ya Newspoll kwa niaba ya jarida la the Australian, imepata kuwa chama cha Labor kina ongoza mseto wa upinzani kwa asilimia 52-48 katika kura ya upendeleo wa vyama viwili, kufuatia bajeti, hiyo ikiwa ni jeki ya asilimia moja tu kutoka mwezi uliopita.
Punguzo ya $300 ya bili ya nishati imekuwa maarufu ambapo asilimia 72 ya watu waki unga mkono hatua hiyo, kulingana na kura ya maoni ya Resolve iliyo simamiwa na gazeti za shirika la habari la Nine. Waziri wa Nishati wa Shirikisho Chris Bowen amesema serikali haijali matokeo ya kura za maoni baada ya bajeti kutangazwa.

Kiongozi wa upinzani Peter Dutton amesema bajeti ya shirikisho haija fanya vyakutosha kupunguza shinikizo za gharama ya maisha nchini Australia. Msingi wa jibu la upinzani wa mseto kwa bajeti ya taifa ilikuwa, pendekezo lakupunguzwa kwa uhamiaji wakigeni, pamoja na mpango waku punguza uhamiaji wakudumu wa kila mwaka kwa kiwango cha watu laki moja elfu arubaini kila mwaka wakishinda uchaguzi mkuu. Serikali ya Labor imekosoa sera hiyo ambayo chama cha Greens ime ita "chuki dhidi ya wageni” ikisema kuwa sera hiyo ita athiri msingi wa uchumi na ujuzi. Bw Dutton amesema kupunguza uhamiaji kuta saidia kupunguza shinikizo kwa soko la nyumba.

Serikali ya New South Wales imesema kukamatwa kwa zaidi ya watu 550 kwa makosa ya unyanyasaji wa nyumbani na familia, ni sehemu ya oparesheni za kawaidi katika miezi 18 iliyopita. Jeshi la polisi la New South Wales limewakamata watu 554 pamoja nakufungua mashtaka 1075, katika siku nne za oparesheni zilizo walenga wahalifu wabaya zaidi jimboni New South Wales wa unyanyasaji wa nyumbani na familia wiki iliyopita. Oparesheni hiyo iliwajumuisha polisi katika vituo vyote, na wilaya za Jimbo ambako watu 226 walikuwa wakisakwa kwa makosa makubwa. Waziri wa Polisi wa jimbo Yasmin Catley ame eleza shirika la habari la A-B-C kuwa, hii ni raundi ya sita tangu oparesheni Amarok Six ilipo anza.

Watoto ambao wana chini ya miaka 16 wanaweza pigwa marufuku kutumia, baadhi ya mitandao yakijamii jimboni New South Wales. Kiongozi wa NSW Chris Minns amesema mitandao yakijamii inaweka shinikizo kwa watoto na serikali iko tayari kukabili swala hilo licha ya kiwango kikubwa cha swala hilo. Serikali ya NSW ita andaa kongamano kujadili madhara yanayo husiana na mtandao wa kijamii na, jinsi yaku shughulikia swala hilo. Bw Minns amesema matumizi ya mitandao yakijamii, imedhuru moja kwa moja afya ya akili ya vijana.

Helikopta iliyokuwa imembeba rais wa Iran Ebrahim Raisi na waziri wake wa mambo ya nje ilianguka siku ya Jumapili ilipokuwa ikivuka eneo la milima katika ukungu mkubwa, wakati ikirejea kutoka kwenye mpaka na Azerbaijan, afisa mmoja wa Iran aliliambia shirika la habari la Reuters. Afisa huyo alisema maisha ya Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amirabdollahian "yako hatarini kufuatia ajali ya helikopta". "Bado tuna matumaini lakini taarifa zinazotoka kwenye eneo la ajali zinatusumbua sana," afisa huyo alisema kwa sharti la kutotajwa jina. Hali mbaya ya hewa ilikuwa ikitatiza juhudi za uokoaji, shirika la habari la serikali IRNA liliripoti.

Jeshi la Uganda limemkamata kamanda wa kundi la waasi linaloshirikiana na Islamic State ambaye ni mtaalamu wa kutengeneza vilipuzi, au mabomu, ambayo kundi hilo limetumia kufanya mashambulizi mabaya katika  siku za nyuma, jeshi lilisema Jumapili. Mpiganaji huyo, Anywari Al Iraq, raia wa Uganda, alikamatwa katika misitu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako kundi la waasi la Allied Democratic Forces lina makao yake, jeshi la Uganda People's Defense Forces, lilisema katika taarifa yake. Wakati wa operesheni hiyo, watu tisa wakiwemo watoto, waliokolewa kutoka

Share