Taarifa ya Habari 20 Februari 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Get the SBS Audio app

Other ways to listen

Waziri Mkuu Anthony Albanese anamshtumu kiongozi wa upinzani wa shirikizo Peter Dutton, kwa kuwahamasisha wasafirishaji haramu wa watu.


Kura mpya ya maoni imedokeza kuwa wa Australia wanaunga mkono kwa upana mageuza mapya ya serikali ya Albanese kwa awamu ya tatu ya makato ya kodi ila, sera hiyo kufikia sasa imefeli kuungwa mkono zaidi. Makato hayo yata wasaidia walipa kodi kupokea makato na asilimia 84 watafaidi pakubwa kuliko ingelikuwa chini ya mfumo wa kwanza wa chama cha mseto.

Watu wanne walipigwa na radi walipokuwa wakijikinga kutoka kwa dhoruba kali katika bustani la Sydney Royal Botanic Gardens jumatatu wana endelea kupata matibabu. Wanne hao walipoteza fahamu kwa muda wakati mingurumo mingi ya radi ilipita juu ya Sydney jana Jumatatu mchana. Dhoruba hiyo ilivyo pita kati ya saa tano asubui na saa nane mchana takriban visa vya radi elfu sabini na tano, vilishuhudiwa ndani ya umbali wa kiilomita 100 ya Sydey na mtandao kamili wa radi na hali ya hewa.

Wanamgambo waliua watu 15 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jimbo la Ituri, vyanzo katika eneo hilo vilisema Jumapili, likiwa shambulio la pili chini ya wiki moja. Vyanzo hivyo vilisema kundi la wanamgambo wa CODECO, ambalo linadai kulinda maslahi ya watu wa kabila la Walendu, kwa mara nyingine lilishambulia watu kutoka kabila hasimu la Wahema.

Rais William Ruto amewakosoa wabunge kwa kutelekeza agenda yake ya kutoa nafasi za ajira zikiwemo nafasi kwenye mataifa ya nje na badala yake amewataka kuunga mkono ajenda hiyo inayonuia kupunguza tatizo la ajira. Akiongoza mkutano wa siku nne wa baraza la mawaziri na viongozi wakuu serikalini ambao unafanyika katika mji wa Naivasha kaunti ya Nakuru, Rais Ruto amechukua fursa hiyo kuwarai viongozi kuwajibika na kuiunga mkono serikali kikamilifu.

Nchini Tanzania kunashuhudiwa upungufu mkubwa wa fedha za kigeni, hasa dola ya Marekani, ambayo ni muhimu kwa biashara ya kimataifa na pia kwa watu wanaotajia kwenda kuhiji mwaka huu




Share