Taarifa ya Habari 19 Machi 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya Albanese imesema itapinga kuachiwa huru kwa zaidi ya watu 100 ambao wako ndani ya kizuizi cha uhamiaji, katika kesi nyingine muhimu itakayo fikishwa mbele ya mahakama kuu.


Raia wa Iran anaye julikana kama ASF17 anafanya zabuni yakisheria kwa uhuru ambayo, akifanikiwa inaweza fanya aachiwe huru pamoja na watu wengine 150. Kesi hiyo inahusu kanuni ya watu waliowekwa kizuizini kwa muda usiojulikana na walio kataa kushirikiana na mamlaka ya Australia.

Familia zawa Australia zitaweza pata miezi sita ya likizo ya wazazi yenye malipo kufikia 2026. Sheria mpya zilizo pitishwa leo zita ona likizo ya wazazi ikiongezwa kwa wiki mbili kila mwaka hadi 2026, wiki 4 za likizo zikitengwa kwa kila mzazi. Hatua nyingine katika mageuzi ya malipo ya likizo ya wazazi, ni kuongezewa kwa malipo ya ustaafu ambayo, chama cha Labor kinatumai kupitisha katika miezi ijayo.

Ni biashara moja tu kati ya 20 nchini Australia ambazo ziko tayari kutumia na akili bandia ya A-I, licha ya utafiti kudokeza karibu kazi zote zita athiriwa kwa mujibu wa ripoti. Ripoti ya nne ya ujuzi wa mtandaoni ya RMIT imesema wafanyakazi tayari wanakumbatia vifaa hivyo, na kuokoa tarikban masaa 5.3 kila wiki kushughulikia kazi za kawaida. Ila, ripoti hiyo imepata kuwa ukosefu "muhimu" wa uelewa kuhusu kuzalisha akili ya bandia.

Kimbunga cha kitropiki katika Wilaya ya Kaskazini, kinatarajiwa kupungua ukali leo Jumanne 19 Machi baada yakufika katika eneo hilo usiku waku amkia. Ofisi ya utabiri wa hewa imesema Kimbunga Megan kina elekea katika nchi kavu kutoka pwani ya Gulf of Carpentaria, na kinatarajiwa hatimae kupungua ukali. Kimbunga hicho haki tarajiwi kugeuka kuwa kimbunga chaki tropiki, hata kama kinaweza elekea pwani ya Magharibi Kimberley baadae wiki hii.

Mashirika kadhaa ya serikali na yale ya kutoa misaada nchini Haiti yameripoti kuwa vifaa vyao, pamoja na misaada imeporwa, huku nchi hiyo ikiingia kwenye wimbi jingine la ghasia za magenge. UNICEF ilisema kuwa kontena la usafirishaji lililojaa vifaa muhimu vya msaada limeporwa huku serikali ya Guatemala ikisema kuwa kituo cha ubalozi pia kiliibiwa.

Wakaazi wenye hasira kutoka Hosteli ya Diepkloof katika kitongoji cha Soweto mjini johanesburg Afrika kusini, wamechoma matairi katika jaribio la kuziba barabara na kuwarushia mawe polisi kufuatia maandamanao ya ghasia ya kupinga ukosefu wa usambazaji wa huduma muhimu na hali mabaya ya makazi.

Waziri wa Uchukuzi na Barabara Kipchumba Murkomen na Seneta wa Nandi, Samson Cherargei wameendeleza uhasama wao, wawili hao ambao ni wandani wa Rais William Ruto wakishambuliana hadharani. Hata baada ya Bw Mukormen kumsihi Cherargei amuombe msamaha na kufutilia mbali madai hayo katika mitandao ya kijamii, Waziri ameeleza katika kesi aliyomshtaki katika Mahakama ya Milimani kwamba Seneta huyo alikataa na “badala yake kumtaka wakutane kortini mbivu na mbichi zijulikane.”


Share