Taarifa ya Habari 19 Februari 2024

City - Swahili.jpg

Get the SBS Audio app

Other ways to listen

Waziri wa mazingira Tanya Plibersek amemshtumu Peter Dutton kwa kuwasaidia wasafirishaji haramu wa watu kufanya matangazo, kwa kudai kuwa serikali ya shirikisho imeregeza hatua za usalama mpakani.


Hali hii imejiri baada ya takriban wanaume 40 kuwasili kwa boti karibu ya jumuiya ya Kijiji cha Beagle Bay cha magharibi Australia. Imeripotiwa kuwa wanaume hao wanatoka Pakistan, India na Bangladesh, kwa sasa wame pelekwa katika kizuizi cha uhamiaji cha Australia ambacho kiko katika taifa la kisiwa cha Nauru. Tangazo hilo limesababisha vita vya maneno kati ya Waziri Mkuu Anthony Albanese na kiongozi wa upinzani wa shirikisho Peter Dutton, ambaye amesema oparesheni za mipaka ya Australia zimeregea chini ya serikali ya Albanese.

Jeshi la polisi nchini Papua New Guinea limesema takriban watu 53 wame uawa katika kile ambacho mamlaka wana amini kina weza kuwa ni mauaji makubwa ya kimbari katika historia ya hivi karibuni ya nchi hiyo. Ina aminika wanaume hao walipigwa risasi nakufa katika hali ambayo polisi wanadai ni shambulizi katika jimbo la Enga, ambayo iko katika milima ya kaskazini ya nchi hiyo. Shirika la habari la ABC limeripoti kuwa jeshi la polisi linatarajia kupata miili mingine, wanapo endelea kufanya msako katika maeneo ya karibu ya tukio. Mamlaka wana amini wanaume hao walishambuliwa walipokuwa waki elekea kuishambulia kabila jirani.

Seneta huru Jacqui Lambie amesema haja shangaa wa Australia wamesema wanaunga mkono mageuzi ya makato ya kodi, ukizingatia shinikizo za gharama ya maisha. Kura mpya ya moani ya makampuni ya Australian Financial Review/Freshwater Strategy imedokeza kuwa wa Australia kwa wingi wana unga mkono mageuzi mapya ya serikali ya Labour kwa awamu ya tatu ya makato ya kodi. Mageuzi hayo ya kodi yatawasaidia walipoa kodi kuokoa hela, wakati 84% ya watu watafaidika zaidi kuliko, wangelifaidika chini ya mfumo wa asili wa chama cha mseto. Kura hiyo ya maoni imeonesha kuwa 44% ya watu wanaunga mkono mageuzi mapya, kulinganisha na 15% wanao upinga.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza maziko ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa taifa hilo Edward Ngoyai Lowassa yaliyofanyika hii leo nyumbani kwake Monduli Arusha na kuudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wanasiasa kutoka vyama vya upinzani.

Akizungumza wakati akitoa salamu za pole kwa familia na wananchi wa Tanzania Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema njia nzuri ya kumuenzi hayati Edward Lowassa ni kufanya siasa za maridhiano na siasa za kujenga hoja, kuheshimiana, kustahamiliana bila kulumbana wala kutikisa misingi ya utaifa. Hata hivyo Rais Samia ameongezea kusema kuwa Lowassa ni kiongozi alieacha funzo kuwa watu wanaweza kutofautiana katika mitazamo na sera bila kuvunja misingi ya Utaifa wao.

Kura ya turufu ya Marekani, itaweza kutumika kuzuia mpango wa Algeria, unaotarajiwa kufikishwa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki hii wa kusitishwa mara moja vita vya Israel, vya Gaza, kwa mujibu wa balozi wa Marekani, wa Umoja wa Mataifa.

Linda Thomas-Greenfield, amesema katika taarifa yake Jumamosi kwamba Marekani imekuwa ikifanyakazi kwa miezi kadhaa juu ya suluhisho endelevu la mzozo wa Gaza ambao utaleta kwa haraka na utulivu endelevu kwa Gaza kuanzia angalau wiki sita, na kisha kuchukua hatua za kujenga amani ya kudumu.

Amesema mpango huo ambao Marekani inaufanyia kazi pamoja na Israeli, Misri na mataifa mengine, unawakilisha fursa bora ya kuwaunganisha mateka wote na familia zao na kuwezesha kusitisha mapigano kwa muda mrefu, kuruhusu chakula zaidi cha kuokoa maisha, maji, mafuta, dawa, na vitu vingine muhimu kuwafikia raia wa Palestina wenye uhitaji.

Katika michezo:

Isaac Cooper na timu ya wanawake ya mbio za mita 100 kwa waogeleaji wanne, wame maliza mashindano yakuogelea yadunia mjini Doha katika hali chanya, baada yakushinda medali mbili za hadhabu kwa niaba ya Australia. Ikiwa na medali za dhabu tatu, tisa za fedha na nne za shaba, Australia ilishinda idadi ya medali 16 na ilishindwa tu na Marekani iliyo shinda  medali 20 medali 8 kati yazo zikiwa niza dhahabu.

Share