Taarifa ya Habari 18 Machi 2024

City - Swahili.jpg

Vizuizi vya uhamiaji vinatarajiwa kutawala siasa za Australia wiki hii wakati serikali ina jiandaa kukabiliana na kesi nyingine ndani ya mahakama kuu, ambako watu wingine 100 wanaweza achiwa huru.


Mwanaume mmoja mwenye asili ya Iran anaye julikana kama A-S-F 17, ambaye amefungwa kwa kukataa kushirikiana na mamlaka wa Iran, ata omba kuachiwa huru kutoka kizuizini ndani ya mahakama kuu mwezi ujao. Akifanikiwa, kesi yake inaweza sababisha watu wengine 151 kuachiwa huru. Mwaka jana, serikali iliharakisha kuwasilisha sheria zakusimamia watu 149 walio achiwa huru kutoka kizuizini kwa masharti makali ya visa, baada ya mafanikio ya kesi ndani ya mahakama kuu inayo julikana kama NZYQ.

Kampuni yaku changia usafiri Uber, imekubali kulipa jumla ya $272 milioni, kwa madereva wa taxi pamoja na wamiliki wengine wamagari yakukodi kufuatia hatua kampuni hiyo iliyo chukua ndani ya soko la Australia. Idadi kubwa ya wafanyakazi ndani ya sekta hiyo, walikuwa wanatarajiwa kupeleka kesi yao dhidi ya Uber katika mahakama kuu ya Victoria, wali amua kusitisha kesi yao baada ya kampuni hiyo kukubali kuwafidia.
Kesi ambayo ingekuwa ya tano kwa ukubwa zaidi nchini, zaidi ya wafanyakazi 8000 walikuwa wanatarajiwa kuwaiwajibisha Uber, kwa kuwafanya wapoteze sehemu kubwa ya mapato yao.

Serikali ime wahamasisha wa Australia wa fanye tahadhari kwa data zoa mtandaoni, wakati Marekani inakaribia kupiga marufuku TikTok. Bunge la Marekani wiki jana, lilipitisha muswada wakupiga marufuku mtandao huo wakijamii, hatua iliyo zua mjadala kuhusu usalama wa TikTok Australia. Seneta wa chama cha Liberal, James Paterson ameomba Australia ichukue hatua hiyo pia. Wakati huo huo, waziri Tanya Plibersek ame eleza kipindi cha Sunrise kuwa serikali inasikiza ushauri wa mashirika ya usalama.

Rais mteule wa Urusi Vladimir Putin amesema kulikuwa majadiliano kutumia kiongozi wa upinzani wa zamani Alexei Navalny katika mabadilisho na wafungwa wengine wa Urusi kutoka nchi za magharibi kabla ya kifo chake. Katika hotuba yake ya kwanza baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais kutangazwa, Bw Putin ali zungumzia swala la kifo cha Bw Navalny akisema ilikuwa bahati mbaya. Bw Navalny, ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa Vladimir Putin, ali uawandani ya gereza la Arctic na baadhi ya watu walisema hakuwa amestahili kufungwa. Bw Putin ameongezea kuwa sharti kuu la mabadilishano ya Bw Navalny na wafungwa hao, ni kwamba angeruhusiwa kurejea Urusi.

Mapigano mapya yamezuka hapo jana kati ya vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 katika mji wa Sake unaopatikana takriban kilometa 20 magharibi mwa mji wa Goma. Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo Bintou Keita amesema askari wanane wa kulinda amani wamejeruhiwa kufuatia mapigano hayo yaliyozuka mashariki mwa Kongo baada ya siku kadhaa za utulivu. Luteni kanali Guillaume Ndjike, msemaji wa jeshi katika jimbo hilo, amevishutumu vikosi vya Rwanda kwa kukilenga kituo cha Umoja wa Mataifa huko Sake wakati wa mapigano hayo. Wiki mbili zilizopita, kundi hilo linaloongozwa na Watutsi la M23 lilianzisha mashambulizi mapya na kuilenga miji kadhaa iliyo karibu na Goma, na hivyo kujizatiti katika maeneo ya kaskazini kama Rutshuru na Masisi.

Share