Taarifa ya Habari 17 Mei 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Kupungua kwa urasimu, bajeti iliyo rahisishwa, na kupungua kwa uhamiaji ni sehemu muhimu ya mpango wa chama cha mseto kwa Australia.


Chama cha Greens kime fanya maafikiano na serikali ya Labor kuondoa utoaji wa njia ya haraka ya sheria ya serikali uchimbaji wa gesi nje ya nchi. Sheria hiyo itajumuisha utoaji ambao utaruhusu waziri wa rasilimali kufanya mageuzi kwa mchakato wakutoa idhini ya gesi, kukwepa mazingira ya ulinzi wa sheria na ushauriano na jumuiya za Mataifa ya kwanza.

Kiwango cha ukosefu wa ajira kimeongezeka nakufika asilimia 4.1 kutoka Aprili hali ambayo imefanya, kuruka juu kwa viwango hivyo tangu Machi wakati kiwango hicho kilikuwa asilimia 3.8. Ongezeko hilo lilikuw juu kuliko ilivyo tabiriwa, kuwa kiwango hicho kitakuwa asilimia 3.9. Data kutoka ofisi ya takwimu ya Australia imeonesha kuwa takriban nafasi za ajira 38,000 ziliwasilishwa katika soko la ajira ndani ya siku 30 za mwisho.

Mahakama ya Juu ya Umoja wa Mataifa, ICJ, imeanza kusikiliza shauri lililowasilishwa na Afrika Kusini ikiitaka kuishinikiza Israel kusitisha operesheni yake ya kijeshi katika mji wa Rafah, kusini mwa Gaza, ambako zaidi ya nusu ya wapalestina wametafuta hifadhi. Afrika Kusini imeiambia mahakama hiyo katika siku ya kwanza ya kusikiliza shauri hilo siku ya Alhamisi, kuwa mauaji ya kimbari yanaendelea Gaza, wakati ambapo Israel ikisema wanajeshi zaidi wataingia Rafah.

Kenya na Uganda zimeafikiana kuweka kando tofauti zao na kuimarisha biashara ya mafuta kati ya nchi hizo mbili. Matiafa hayo yamekubaliana kujenga bomba la mafuta kutoka Eldoret hadi Kampala na pia kusafirisha bidhaa hiyo moja kwa moja kupitia Nairobi. Makubaliano haya yanajiri katika ziara rasmi ya Rais Yoweri Museveni nchini Kenya inayodhamiria kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.

Watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania wameitaka serikali ya nchi hiyo kubuni sheria maalum kwa ajili ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kutokana na kuwepo kwa ongezeko la kubwa la ukatili katika kipindi cha hivi karibuni hali inayoendelea kutia wasiwasi. Huku watetezi hao wakisema sheria iliyopo bado ina mapungufu yanayoendelea kutoa nafasi ya wanawake kuendelea kufanyiwa ukatili.

Wachezaji watatu wa ligi kuu ya soka Australia wafunguliwa mashtaka ya kucheza kamari na jeshi la polisi la New South Wales.

Share