Taarifa ya Habari 16 Februari 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Get the SBS Audio app

Other ways to listen

Upinzani wa shirikisho una wasiwasi kuhusu hali ya uchumi wa Australia, kiwango cha ukosefu wa ajira kikiongezeka hadi 4.1%.


Watoaji wa huduma ya afya binafsi wanaomba mageuzi kwa sheria, kuboresha matokeo ya ugonjwa wa kisukari kwa wagonjwa. Kama sehemu ya uchunguzi kwa ugonjwa wa kisukari nchini Australia, shirika la Private Healthcare Australia limeomba serikali ibadili sheria za sekta hiyo kuruhusu wauguzi watoe mipango ya usimamizi wa magonjwa sugu.

Takriban nyumba 44 zime teketezwa kwa moto katika eneo la Pomonal katika Mbuga ya kitaifa ya Grampians jimboni Victoria ambako kuna hofu kuwa idadi hiyo inaweza ongezeka kulinga na taarifa kutoka kwa kiongozi wa jimbo hilo Jacinta Allan. Nyumba moja ilipotezwa pia katika eneo la Dadswells Bridge.

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Afrika wanakutana mjini Addis Ababa kwa mkutano wao wa 44 kutayarisha mkutano wa kilele wa 37 ambao viongozi watajadili suala la mfumo wa elimu barani humo pamoja na migogoro ambayo inasababisha hali ya ya wasi wasi katika sehemu nyingi za bara hilo.

Waziri wa nishati wa Uganda Ruth Nankabirwa amesema nchi hiyo inafanya mazungumzo na Tanzania ili kusafirisha bidhaa zake zote za mafuta kupitia Dar es Salaam. Hii ikimaanisha hawataitumia bandari ya Mombasa, Kenya. Uganda haijaridhishwa na mfumo wa muda mrefu ambao kampuni za mafuta za Uganda hununua asilimia 90 ya bidhaa zao kupitia kampuni tanzu za nchini Kenya.

Mamia ya wanawake wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo waliandamana siku ya Jumatano mjini Kinshasa wakitaka vita kukomeshwa huko mashariki mwa nchi yao ambako mapigano yamezidi katika siku za hivi karibuni kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa M23.


Share