Taarifa ya Habari 15 Machi 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mamlaka jimboni Victoria wame zindua uchunguzi kwa mgodi ulio bomoka mjini Ballarat naku uwa mwanaume mmoja pamoja nakumuacha mwingine akipigania maisha yake.


Mdhibiti wa mazingira jimboni New South Wales amesema, uchunguzi wayo kwa mbolea iliyo jaa kemikali zenye asbestos katika sehemu kadhaa mjini Sydney utaendelea, wakati serikali inafanya maandalizi yakuongeza mamlaka yake. Chini ya mageuzi hayo, mamlaka ya ulinzi wa mazingira ya jimbo, itapewa mamlaka ya ziada kuwafungulia mashtaka watu binafsi namakampuni, yanayo feli kutupa asbestos katika hali sahihi, wakati adhabu kwa makosa hayo yatakuwa mara mbili zaidi kwa maana ya milioni 10 kwa makampuni.

Uchambuzi mpya umedokeza kuwa matumizi ya wanafunzi wakimataifa yame changia kwa zaidi ya ukuaji wa nusu ya pato la taifa la Australia mwaka jana. Uchambuzi huo ulio fanywa na wachumi wa NAB, umesema michango yao ili saidia uchumi kuepuka robo mbili mfululizo za ukuaji hasi wa uchumi, naku uondoa kutoka mdororo wakiufundi. Ila mchango huo unatarajiwa kupungua wakati utoaji wa viza za wanafunzi tangu 2022, zaidi ya viza 90,000 zilitolewa katika robo ya mwisho.

Chama tawala cha Afrika Kusini, ANC kinasema kina uhakika kitaendelea kuwa na wingi wa viti kwenye bunge la taifa wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Mai na kwamba hakijaanza mazungumzo na chama kingine cha kisiasa juu ya uwezekano wa kuunda serikali ya mungano.

Wagonjwa wamekwama katika hospitali mbalimbali nchini Kenya kufuatia mgomo wa madaktari unaolenga kuwezesha utekelezaji wa mahitaji ya nafasi za lazima za mafunzo ya utabibu kwa zaidi ya madaktari waliohitimu 4,000, ajira na mazingira bora ya kazi.

Serikali na hospitali binafsi nchini Tanzania zimetakiwa kutafuta njia za kupunguza gharama za matibabu ya figo na kuboresha huduma za Afya kwa wagonjwa wanaohitaji matibabu hayo. Wakizungumza na vyombo vya habari, baadhi ya wagonjwa na wadau wa afya wametoa wito huo kuhakikisha wagonjwa wa figo wanapata matibabu na kisha matibabu hayo kuingizwa kwenye mfuko wa bima ya Afya.

Share