Taarifa ya Habari 14 Machi 2024

City - Swahili.jpg

Polisi wame pata mwii wa mwanaume aliye fariki ndani ya mgodi ulio bomoka Ballarat, katika kanda ya Victoria.


Mwanaume huyo mwenye miaka 37 alikuwa mmoja kati ya wanaume wawili walio gongwa na mawe yaliyo kuwa yakianguka ndani ya mgodi huo katika eneo la Mount Clear. Katibu wa jimbo wa chama cha wafanyakazi wa Australia Ronnie Hayden, amesema mwanaume mwingine kwa sasa huko katika hali mbaya hospitalini. Ame ongezea kuwa kila mtu ame huzunika.

Serikali ya shirikisho ime zindua mradi wa majaribio katika jimbo la Kusini Australia, ambao uta watumia wauguzi watendaji kutoa huduma ya kwanza ya afya. Mradi huo wa majaribio uta ipa fursa serikali ya madola kuwekeza kwa wauguzi watendaji ambao wata hudumu katika zahanati zama GP katika jimbo hilo. Waziri wa Afya washirikisho Mark Butler amesema anatumai mradi huo wamajaribio utaonesha kuwa kuwatumia wauguzi watendaji, kuna weza ondoa shinikizo kwa idara za dharura na zahanati zama GP ambazo ziko tayari chini ya shiniko.

Kiongozi wa genge la wahalifu na mwenye ushawishi mkubwa nchini Haiti ameahidi kuendeleza mapambano yaliyolitumbukiza taifa hilo katika machafuko. Jimmy Cherizier maarufu kama "Barbecue," amesema jana Jumatano kwamba muungano wake wa magenge yenye silaha "haujali juu ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Ariel Henry." Henry aliachia ngazi baada ya mkutano wa dharura siku ya Jumatatu na nafasi yake kuchukuliwa na Baraza Tawala la mpito. Barbecue aliyekuwa afisa wa polisi amesisitiza kwamba wataendeleza mapambano ya ukombozi wa Haiti. Haiti haijafanya uchaguzi wa kitaifa tangu 2016, na hakuna bunge wala rais. Nafasi ya Rais Jovenel Moise, aliyeuawa 2021, haijajazwa na Henry amekuwa akiongoza nchi hiyo tangu kifo chake.

Rais wa Nigeria aliamuru maafisa wa usalama kutolipa fidia kwa ajili ya kuachiliwa kwa zaidi ya wanafunzi 250 wa shule ya msingi waliotekwa nyara na watu wenye silaha wiki iliyopita, waziri wa habari alisema Jumatano. Ndugu wa wanafunzi hao wanasema watekaji nyara wameomba fidia kubwa ili kuwaachilia wanafunzi waliotekwa nyara shuleni mwao Alhamisi iliyopita katika kijiji cha Kuriga kaskazini magharibi mwa jimbo la Kaduna. Magenge ya wahalifu mara nyingi huteka nyara watu wengi kaskazini mwa Nigeria, yakilenga shule, vijiji na barabara kuu.

Katika michezo:

Mwalimu mpya wa timu ya taifa ya Japan katika mchezo wa raga ya wanaume Eddie Jones, amesema anapanga kufanya timu yake kuwa moja ya nne bora duniani. Bw Jones anachukua mikoba ya uongozi wa Japan, kwa mara ya pili baada ya kufunza Australia kwa muda mfupi na kabla ya hiyo alifunza England kwa miaka saba. Amesema timu yake inastahili unda aina yakucheza inayo faa sifa zaki Japani

Na katika soka, Central Coast Mariners FC wanajiandaa kupeperusha bendera ya Australia katika mechi ya pili ya nusu fainali ya kombe la klabu bingwa Asia dhidi ya Odisha FC ya India. Central Coast Mariners walishanda mechi ya kwanza kwa goli 4 sufuri.

Na katika taarifa za hali ya hewa:

Adelaide nyuzi joto, 26
Brisbane nyuzi joto, 30
Canberra nyuzi joto, 29
Darwin nyuzi joto, 30
Hobart nyuzi joto, 19
Melbourne nyuzi joto, 22
Perth nyuzi joto, 31
Sydney nyuzi joto, 30

Share