Taarifa ya Habari 12 Machi 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali imesema imetupilia mbali kutumia ushuru kuwekeza mfumo wa malezi ya wazee, baada yakutolewa kwa ripoti ya nguvu kazi katika sekta hiyo.


Nguvu kazi hiyo imesema kuwa serikali ya madola ita endelea kuwa mwekezaji mkuu wa huduma za malezi ya wazee katika siku za usoni, wakati umma unaendelea kuzeeka na mahitaji ya huduma hizo yakiongezeka. Imependekeza wastaafu watumie hela zao zaustaafu, kusawazisha malipo ya huduma za malezi ya uzeeni kuondoa shinikizo kwa mikoba ya serikali ya madola.

Upinzani wapekee wa Labor nchini, unaonekana kukabiliana na pambano gumu wakati wakati tarehe ya uchaguzi wa jimbo hilo inakaribia. Kura ya maoni ya hivi karibuni imedokeza kuwa chama cha Labor kina ungwa mkono na asilimia 26 yawapiga kura, kabla ya uchaguzi wa Machi 23 ambapo chama tawala cha Liberal kina wania awamu ya nne ya uongozi. Iwapo upigaji kura utafuata madokezo ya kura ya maoni, moja kati ya chama cha Liberal au Labor hakita kuwa na viti vyakutosha kuunda serikali ya wengi.

Tathmini huru kwa kwa ushuru wa barabara za New South Wales, umeomba urekebishaji kamili wa mtandao wa ushuru wa barabara ambao kwa sasa unawagharimu madereva wa Sydney bilioni 2.5 ya dola kila mwaka. Chini ya mapendekezo ya mageuzi kwa mzigo wa ushuru wa barabara wa dola bilioni 123 mjini humo, ushuru wa barabara unaweza pungua kote mjini Sydney ila madereva wata kabiliwa kwa ushuru wa barabara kwenda nakurudi kupitia daraja maarufu la Habour Bridge. Sheria mpya zinazo tekelezwa chini ya mapendekezo, zinaweza iweka serikali katika kiti chamadereva inapokuja kwa bei, kwa matumaini kuwa gharama inaweza badilika kutoka vitongoji vya wafanyakazi kwa wale wanao ishi katika vitongoji vyakifahari vya mashariki na kaskazini ya Sydney.

Ripoti mpya imedokeza viwango vya juu vya shinikizo yakukodi nchini kwa sasa, vinapatikana katika majimbo ya Magharibi Australia na Queensland. Kielezo cha maumivu ya kukodi kutoka kundi la nyumba kwa jina la SuburbTrends kimeonesha kuwa kuna viwango visivyo vya kawaida vya magumu yakifedha kote nchini, wakati gharama ya nyumba inaendelea kuongezeka zaidi ya pendekezo la kiwango cha asilimia cha mapato kwa watu. Ripoti hiyo imesema kuwa majimbo ya Magahribi Australia na Queensland, yana ongoza taifa katika ugumu wakukodi wakati kuna vitongoji vingi vinavyo kabiliana na viwango vya juu vya shinikizo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito wa kuwekwa chini silaha katika vita vya Israel huko Ukanda wa Gaza na pia kwenye mzozo nchini Sudan wakati mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhani ukianza. Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alitoa pia wito wa kuachiwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas na kuondolewa kwa vizingiti vyote ili kuhakikisha upelekaji wa misaada ya dharura katika kasi na kiwango kikubwa kinachohitajika Gaza. Umoja wa Mataifa unaonya kuwa robo ya wakaazi wako ukingoni mwa kukabiliwa na njaa.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Angola tete Antonio amesema Jumatatu jioni kwamba Rais Paul Kagame wa Rwanda amekubali kukutana na mwenzake wa Jamhiri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mazungumzo kuhusu hali ya usalama mkashariki ya Congo. Ofisi ya rais wa Rwanda kwenye ujumbe wake katika ukurasa wake wa X imeeleza kwamba wakuu hao wamekubali juu ya hatua muhimu kuelekea kutanzua sababu msingi wa ugomvi na haja ya kuheshimu utaratibu wa makubaliano ya Luanda na Nairobi wa kupatikana Amani na utulivu katika kanda nzima.

Takriban mtu mmoja amefariki baada ya mlipuko kutokea kwenye maduka kadhaa katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu. Mlipuko wa Jumapili ulikuwa wa pili kulikumba soko maarufu la Bakara katika muda wa mwezi mmoja tu. Ni soko kubwa sana mjini Mogadishu na ambako wakazi wengi hupata mahitaji yao ya vyakula, nguo, dawa, vifaa vya elektroniki na vitu vingine.

Share