Taarifa ya Habari 11 Machi 2024

City - Swahili.jpg

Polisi wamesema juhudi zakumtafuta mvulana wa miaka 12 katika eneo la magharibi Sydney, zimefika katika hatua muhimu wasiwasi kuhusu ustawi wake ukiendelea kuongezeka.


Hussein Al Mansoory haja onekana kwa zaidi ya masaa 48, baada yakupotea mida ya asubuhi ya Jumamosi 9 Machi.
Mvulana huyo mwenye miaka 12, ana ugonjwa wa  down syndrome na autism, na hawezi ongea. Polisi wame sema mvulana huyo anakabiliwa kwa mazingira magumu.

Mweka hazina wa taifa Jim Chalmers ametangaza kuwa serikali inafuta takriban ushuru 500 zinazo zua kero, kwa badhii mbali mbali zinazo jumuisha machine zakufulia, viatu pamoja na vifaa vya kike vya usafi. Ushuru wa kero, ni ushuru ambao uko chini sana kiasi kwamba una igharimu serikali zaidi ku ukusanya kuliko mapato inayo rejesha. Serikali imetangaza itakata asilimia 5 ya ushuru kwa bidhaa 500 zinazo ingizwa nchini, kama sehemu ya kile ambacho Dr Chalmers amesema ni geuzi kubwa zaidi kwa mfumo wa ushuru katika miongo. Katika hotuba kwenye kongomano la shirika la Financial Review Business Summit, alisema kuondoa ushuru huo kuta rahisisha biashara ya kila mwaka yenye thamani ya takriban dola bilioni 8.5.

Wapalestina wanajiandaa kwa mfungo wa Ramadhan katika hali ya huzuni na hatua zilizoimarishwa za usalama na polisi ya Israel. Mazungumzo ya kupatikana muafaka wa kusitishwa mapigano yamekwama. Maelfu ya polisi wamewekwa katika mitaa ya Mji Mkongwe wa Jerusalem, ambako maelfu ya waumini wanatarajiwa kila siku kufika katika eneo la Msikiti wa Al Aqsa, mojawapo ya maeneo takatifu zaidi katika dini ya kiislamu. Eneo hilo, linalozingatiwa kuwa takatifu zaidi na Wayahudi wanaoliita Mlima wa Hekalu au Temple Mount katika Kiingereza, limekuwa kitovu cha msuguano kati ya Israel na Wapalestina.

Kiongozi wa DAP Kenya, Eugene Wamalwa amekataa kupokea marupurupu ya kushiriki vikao vya Kamati ya Kitaifa ya Maridhiano (NADCO) ambayo yanakadiriwa kuwa zaidi ya Sh1milioni. Bw Wamalwa ambaye alikataa kutia saini ripoti ya mwisho ya Nadco kwa msingi kuwa haikutatua kupanda kwa gharama ya maisha, mnamo Ijumaa, Machi 8, 2024 aliandikia Makarani wa Seneti na Bunge la Kitaifa akikataa kulipwa pesa hizo. Mnamo Ijumaa Bw Wamalwa pia hakuwepo wakati wa kuwasilishwa kwa ripoti hiyo kwa Kinara wa Azimio Raila Odinga kwenye afisi zake za Capitol Hill, Nairobi. Pia hakuwepo kwenye Ikulu wakati ambapo wanakamati waliwasilisha ripoti hiyo kwa Rais William Ruto.KIONGOZI wa DAP Kenya, Eugene Wamalwa amekataa kupokea marupurupu ya kushiriki vikao vya Kamati ya Kitaifa ya Maridhiano (NADCO) ambayo yanakadiriwa kuwa zaidi ya Sh1milioni.

Katika michezo,
Nyota wa timu ya taifa Martin Boyle yuko katika hali utulivu hospitalini, baada yakupata jeraha la kichwa katika mechi ya rombo fainali ya kombe la uskochi ambako timu yake ilishindwa na wapinzani wao Rangers. Mchezaji huyo ali ondolewa uwanjani kwa machela baada yakuanguka vibaya, alipo kuwa aki pambania mpira wa hewani na mpinzani wake John Souttar.
Jeraha hilo litazua wasiwasi kwa mwalimu wa timu ya taifa Socceroos Graham Arnold, siku chache kabla ya mechi yakufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Lebanon mjini Sydney 21 Machi.

Katika taarifa za hali ya hewa;

Adelaide nyuzi joto ni 38
Brisbane nyuzi joto ni 29

Canberra nyuzi joto ni 31
Darwin nyuzi joto ni 31
Hobart nyuzi joto ni 26

Melbourne nyuzi joto ni 38
Perth nyuzi joto ni 31
Sydney nyuzi joto ni 29


Tembelea www.sbs.com.au/swahili

Share