Taarifa ya Habari 1 Machi 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili.jpg

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Shirika la ujasusi la Australia limetetea uamuzi wayo wakuto weka wazi jina la mwanasiasa wa zamani ambaye ame husishwa na kundi la ujasusi lakigeni.


Kiongozi mkuu wa ASIO Mike Burgess amesema ni mazoea ya muda mrefu ya shirika hilo la ujasusi, yakuto jadili hadharani maswala ya oparesheni zayo.

Serikali ya Victoria imefuta mlo rasmi wa Iftar wa mwaka huu baada ya mashirika 100 yaki Islamu kuandika barua ya wazi iliyo weka wazi wata susia tukio hilo. Kume kuwa wito sawia huo jimboni NSW na shutma kuwa serikali ya Minns, imeonesha kutojali dhiki yawa Islamu na jumuiya zawa Arabu jimboni humo.

Wachunguzi wame anza kuchunguza kilicho sababisha moto katika eneo la Magharibi Victoria, ulio tishia zaidi ya nyumba 100 kabla hauja dhibitiwa. Moto huo katika eneo la Dereel, kusini Ballarat, uliwaka Jumatano wakati wa hali mbaya ya mazingira. Rick Nugent ni kamishna wa usimamizi wa dharura Victoria, amesema kuna wasiwasi moto huo uliwashwa kimakusudi.

Rais mstaafu wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, alifariki dunia Alhamisi katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya saratani ya mapafu. Mwinyi alikuwa Rais wa pili wa Tanzania alieongoza kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia mwaka 1985 hadi 1995 huku akiwa ni rais wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia baada ya utawala wa chama kimoja.

Mahakama ya Rufaa ya London nchini Uingereza, imeamuru kuwa Rais wa Msumbuji Filipe Nyusi hawezi kushtakiwa nchini Uingereza kuhusiana na tuhuma za kupokea hongo. Jaji Julian Flaux amesema katika uamuzi ulioandikwa kuwa Nyusi ana kinga ya kushtakiwa katika mahakama za Uingereza wakati akiwa rais wa Msumbuji

Mungano wa asasi za kiraia nchini Senegal umetangaza kuundwa kwa mungano mpya na vyama vya kisiasa ili kutayarisha uchaguzi wa rais kabla ya tarehe 2 mwezi Aprili. Katika taarifa yake mungano wa asasi za kiraia Aar Sunu Election, imesema umoja huo mpya utaruhusu kuendeleza hatua na juhudi za pamoja kuzuia juhudi za mapinduzi ya kikatiba yaliyopangwa na serikali.

Share