Kando na upungufu wa chakula, hali ya usalama ina endelea kuwa mbaya wakaazi waki kosa uhakika wa hatma yao kwa sababu ya mapigano.
Profesa Chacha Nyaigotti-Chacha ni mtaalam wa diplomasia katika ukanda wa Afrika Mashariki. Katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, alifunguka kuhusu baadhi ya suluhu kwa mgogoro kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rwanda na DR Congo.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.